Jinsi Ukraine ilivyotekeleza shambulizi dhidi ya ndege 40 za Urusi

Chanzo cha picha, Source in the SBU
Kwa mujibu wa vyanzo ndani ya kitengo cha SBU vilivyozungumza na idhaa ya Ukraine ya BBC, maelezo ya ziada jinsi kitengo hicho maalum cha Ukraine kilivyopanga na kutekeleza shambulizi la kutumia ndege zisizo na rubani dhidi ya kambi za jeshi la angani la Urusi.
Kulingana na SBU, kutokana na shambulizi hilo kwenye kambi hizo nne za jeshi la angani, ndege muhumi 41 za kivita za Urusi ziliharibiwa.
Mamlaka nchini Urusi zimethibitisha kwamba ndege zisizo na rubani zilishambulia maeneo ambayo kambi mbili za jeshi la angani zipo, ila hawajazungumzia hasara iliyopatikana hasa kwenye ndege za kivita.
Vyanzo ndani ya SBU vimesema kwamba , operehsni iliyotekelezwa mapema leo, ilipangwa kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja unusu, na kusimamiwa kibinafsi na Rais wa Ukraine Volodomyr Zelensky na kutekelezwa na mkuu wa usalama nchini Ukraine Vasyl Malyuk na wahudumu wa majukumu maalum.
Aidha vyanzo hivyo ndani ya SBU vimethibitisha kwamba ndege zisizo na rubani kutoka Ukraine zilikuwa zikipaa angani kutoka kwa malori ambayo yaliendeshwa hadi nje ya kambi hizo za kijeshi.
“SBU ilituma ndege hizo zisizo na rubani za aina ya FPV hadi Urusi, na kisha baadae kutuma nyumba za mbao ambazo zinaweza kusafirhishwa,” ripoti hiyo ilisema.”
Baadaye, zilipowasili katika himaya ya Urusi, ndege hizo zilifichwa chini ya paa za nyumba hizo ambazo zilikuwa zimewekwa juu ya Malori.
Na wakati mwafaka ulipofika, paa za nyumba hizi zilifunguliwa kwa mbali na ndege hizo kulenga silaha za kurusha makombora za Urusi.”
Wakati huo huo, vyanzo vingine vya SBU vimedai kwamba “walioshiriki katika shambulizi hilo maalum ya kijeshi wamekuwa Ukraine kwa muda mrefu sana.”
Idhaa ya Ukraine ya BBC pia imepata picha za wakati ambapo ndege hizo zilipotekeleza shambulizi hilo.
Kwa misingi ya hali ya vita hivi, BBC haiwezi kuthibitisha uzito wa taarifa kutoka kwa maafisa wa serikali ya mataifa hayo mawili.