window.__reverb = {}; window.__reverb.__reverbLoadedPromise = new Promise((resolve, reject) => { window.__reverb.__resolveReverbLoaded = resolve; window.__reverb.__rejectReverbLoaded = reject; }); window.__reverb.__reverbTimeout = setTimeout(() => { window.__reverb.__rejectReverbLoaded(); }, 5000);

Kiongozi wa AFC/M23 wakutana na Kabila 'kujadili amani, na utengamano' DRC

Rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila amefanya mazungumzo na kiongozi wa muungano wa AFC/M23 Corneille Nangaa mjini Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini lililopo mashariki mwa nchi hiyo.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo haya ya mubashara kwa leo, tukutane tena hapo kesho.

  2. Kiongozi wa AFC/M23 wakutana na Kabila 'kujadili amani, utengamano' wa DRC

    g

    Chanzo cha picha, @CNangaa

    Rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila amefanya mazungumzo na kiongozi wa muungano wa AFC/M23 Corneille Nangaa mjini Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini lililopo mashariki mwa nchi hiyo.

    Baadaye Nangaa alituma ujumbe kwenye mtandao wa X, uliosema: ulikua ni mkutano mzuri.

    Kulinga ana kiongozi huyo wa waasi ‘’ kulikuwa na mazungumzo ya kutafakari jinsi ya kuimarisha amani ya kudumu, utengamano wa kitaifa na kuishi maisha ya kudumu pamoja’’

    Joseph Kabila alionekana kwa mara ya kwanza hadharani katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi mashariki mwa nchi hiyo yenye machafuko siku ya Alhamisi, akikutana na viongozi wa kidini katika kile ambacho washiriki walisema ni kushinikiza amani.

    h

    Chanzo cha picha, @CNangaa

    g

    Chanzo cha picha, @CNangaa

    Kabila, ambaye amekuwa nje ya nchi tangu mwaka 2023, anasakwa nchini Congo kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa kuunga mkono uasi wa mashariki, ikiwa ni pamoja na kuhusika katika mauaji ya raia.

    Congo pia imechukua hatua ya kusimamisha chama chake cha kisiasa na kunyakua mali ya viongozi wake.

    Kambi ya rais huyo wa zamani inakanusha uhusiano wowote na waasi wa M23 ambao wameteka maeneo mengi zaidi kuliko hapo awali tangu Januari. Hapo awali Bw Kabila alielezea kurejea katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati kusaidia kutafuta suluhu la mzozo huo.

    Serikali ya Rais wa Congo Felix Tshisekedi mjini Kinshasa wiki hii ilimshutumu Kabila kwa "kujiweka kama kiongozi wa waasi"

    Unaweza pia kusoma:

  3. Magwiji watatu wa soka watua Somalia

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Magwiji watatu wa kandanda barani Afrika, Emmanuel Adebayor, Samuel Eto'o na Jay Jay Okocha, wamesafiri hadi mji mkuu wa Somalia kushiriki katika mechi ya maonyesho ambayo wachezaji na maafisa wanatumai kuwa itafungua njia kwa nyota hao wakuu kurejea mara kwa mara.

    "Onyesho hili la kandanda kwa kweli ni wakati wa kihistoria, ni siku ambayo Somalia ilichukua nafasi yake katika hatua ya dunia," alisema kocha wa vijana wa eneo hilo Abdullahi Geesey, akizungumza na BBC Somali.

    "Kushiriki uwanja na Okocha, Eto'o na Adebayor, kuvaa jezi moja na hata kufunga mabao, ni ndoto iliyotimia."

    Picha ambayo wageni hawa wataichukua ni ya Somalia yenye amani, watu walioungana na utamaduni wa kandanda ambao umefufuka.

    "Somalia inastahili kuaminiwa kuanza kuandaa tena michezo katika nchi yao."

    Mshambulizi wa zamani wa Arsenal na Real Madrid, Adebayor alisifu hatua hiyo, ambayo ilikuwa sehemu ya maandamano ya amani yaliyoungwa mkono na shirikisho la soka duniani Fifa, na kuyataja kuwa ya ajabu.

    Maelfu ya watu waliohudhuria walionyesha hali ya uchangamfu kwenye uwanja huo hali ambayo ilionyesha Somalia ya enzi ya zamani.

    "Ninajua kidogo kuhusu Somalia," alisema mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Togo mwenye umri wa miaka 41.

    "Tunakuombea kwa Mungu akupe amani ili uweze kuijenga nchi yako." Aliendelea.

    Hali ya usalama nchini Somalia bado ni ya wasiwasi, na hali katika uwanja huo ilikuwa ya wasiwasi, huku polisi wengi wakilinda uwanja huo.

    Unaweza pia kusoma:

  4. Norway yasema basi ‘imetosha’ kwa wanafunzi wanaosherehekea wiki nzima kumaliza masomo

    h

    Chanzo cha picha, Shutterstock

    Maelezo ya picha, Wahitimu wa shule kutoka Norway wakiwa wamevalia ovaroli nyekundu huonekana mara kwa mara katika siku ya kitaifa ya Norway tarehe 17 Mei.

    Wahitimu wa shule kutoka Norway wakiwa wamevalia ovaroli nyekundu wamekuwa wakionekana Norway

    Baada ya miaka 13 ya shule, Selma Jenvin-Steinsvag na mwanafunzi mwenzake Aksel walikuwa wakikimbia kupanda treni ya Oslo wakiwa wamevalia ovaroli nyekundu. "Baada ya hapo mitihani yetu yote iliyoandikwa itafanywa," alisema Selma, 18.

    Kuonekana kwa wahitimu wa shule, wanaojulikana hapa kama russe , wakitembea huku wamevaa ovaroli za rangi ni jambo la utamaduni wa kizamani ambao huchangamsha wiki kadhaa kabla ya siku ya kitaifa ya Norway tarehe 17 Mei.

    Hii ni alama ya siku ya baada ya mitihani yao kusherehekea mwisho wa maomo yao. Lakini idadi kubwa ya vijana wa Norway, sherehe zimekuwa zikianza wiki mapema, kabla ya mitihani yao kumaliza.

    Na kuna upande mmoja wa sherehe ambao umezidi kuwatia wasiwasi wazazi pamoja na wanasiasa ni - the russebuss .

    "Ni basi la sherehe! Tunatoka nje kila usiku kwa mwezi, tunalewa, tunacheza na marafiki zetu na ni furaha tu!" Anasema Edvard Aanestad mwenye umri wa miaka 19, ambaye anamaliza shule upande wa magharibi wa Oslo.

    Hofu ni kwamba wiki zote za karamu pamoja na shinikizo la rika linalohusika vina athari mbaya kwa ustawi wa jumla wa vijana, pamoja na alama zao.

    " Russebuss huendesha gari usiku kucha kutoka usiku wa manane hadi mapema asubuhi. Tunacheza muziki wenye sauti kubwa sana na sherehe usiku kucha," anasema rafiki wa Edvard, Henrik Wathne, mwenye umri wa miaka 18.

    Sambamba na furaha hiyo, kumekuwa na malalamiko kuwa sherehe hizo husababisha unywaji pombe kupita kiasi, matumizi ya dawa za kulevya na kulala kidogo. Pia kuna wasiwasi kwamba vijana wengi wanahisi kutengwa kwa sababu hawawezi kumudu gharama.

    Na yote kwa sasa yanaendana na kipindi cha mitihani.

    Waziri Mkuu wa Norway Jonas Gahr Store alisema mwaka jana kwamba yeye pia alifurahia kuhitimu kwake, lakini utamaduni wa mabasi ya chama ulikuwa umetoka nje ya udhibiti.

  5. Dawa ya saratani ya majaribio yafanikiwa kuongeza muda wa kuishi maradufu

    h

    Chanzo cha picha, Laura

    Maelezo ya picha, Laura ameishi miaka 6 baada ya kupewa fursa ya muda mfupi kuishi

    Mamia ya maelfu ya watu walio na saratani ya kichwa na shingo iliyoendelea wanaweza kuishi kwa muda mrefu bila saratani yao kurudi kutokana na dawa ya kinga, jaribio la kimatibabu linaeleza.

    Hii ni ishara ya kwanza ya mafanikio kwa wagonjwa walio na saratani hii ambayo ni ngumu kutibu kwa miaka 20, wanasema wanasayansi nyuma ya utafiti.

    Laura Marston, 45, kutoka Derbyshire, anasema "anashangaa bado yuko hapa" baada ya kupewa taarifa "mbaya" kuhusu kuishi kwangu kufuatia kugunduliwa kwa saratani ya ulimi miaka sita iliyopita.

    Alipata matibabu ya kinga kabla na baada ya upasuaji, ambayo watafiti wanasema husaidia mwili kujifunza kushambulia saratani ikiwa inarudi.

    Saratani kichwani na shingoni ni ngumu kutibu na kumekuwa na mabadiliko kidogo katika jinsi wagonjwa wanavyotibiwa katika miongo miwili.

    Zaidi ya nusu ya wale waliogunduliwa na saratani ya kichwa na shingo iliyoendelea hufa ndani ya miaka mitano.

    Laura alipewa nafasi ya 30% tu ya kuishi muda mrefu baada ya kugunduliwa mnamo 2019, baada ya kuwa na kidonda kwenye ulimi ambacho hakingeisha.

    Hatua iliyofuata ilikuwa upasuaji mkubwa wa kuondoa ulimi wake, pamoja na uvimbe kwenye shingo yake, kisha ikambidi ajifunze kuzungumza na kula tena.

    "Nilikuwa na umri wa miaka 39 na nilihuzunika sana," aliambia BBC News.

    Kama sehemu ya utafiti wa kimataifa kuhusu njia mpya za kutibu saratani hiyo, iliyohusisha wataalam kutoka Taasisi ya Utafiti wa Saratani huko London, Laura alikuwa mmoja wa wagonjwa zaidi ya 350 waliopewa dawa ya kinga ya kinga ya pembrolizumab kabla na baada ya upasuaji ili kuimarisha ulinzi wa mwili.

    Unaweza pia kusoma:

  6. Mwanasayansi wa Ufaransa aliyegundua kidongo cha kuavia mimba afariki

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Dk Etienne-Emile Baulieu alisaidia 'kuwezesha uhuru wa wanawake', alisema rais wa Ufaransa

    Mwanasayansi wa Ufaransa aliyetengeneza kidonge cha kutoa mimba amefariki akiwa na umri wa miaka 98.

    Étienne-Émile Baulieu alisaidia kutengeneza dawa ya kumeza ya RU-486, ambayo pia inajulikana kama mifepristone, ambayo imewapa mamilioni ya wanawake ulimwenguni kote njia mbadala salama na ya bei nafuu ya utoaji mimba kwa upasuaji.

    Dk Baulieu alikufa nyumbani kwake huko Paris mnamo Ijumaa, mjane wake alithibitisha katika taarifa.

    Simone Harari Baulieu alisema: "Utafiti wake uliongozwa na dhamira yake ya maendeleo kupitia sayansi, kujitolea kwake kuwapa uhuru wanawake na hamu yake ya kumuwezesha kila mtu kuishi maisha bora na marefu."

  7. Mahakama ya Juu yamruhusu Trump kufuta hadhi ya kisheria kwa wahamiaji 500,000

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Utawala wa Rais Donald Trump sasa unaweza kufuta hadhi ya kisheria ya zaidi ya wahamiaji 500,000 wanaoishi Marekani, Mahakama ya Juu ya Marekani ilitoa uamuzi siku ya Ijumaa.

    Uamuzi huo umesimamisha agizo la jaji wa shirikisho la awali la kuzuia utawala kusitisha mpango wa uhamiaji wa ulioanzishwa na Rais wa zamani Joe Biden. Mpango huo uliwalinda wahamiaji wanaokimbia machafuko ya kiuchumi na kisiasa katika nchi zao.

    Agizo hilo jipya linaweka takriban wahamiaji 530,000 kutoka Cuba, Haiti, Nicaragua na Venezuela katika hatari ya kufukuzwa nchini.

    Majaji Ketanji Brown Jackson na Sonia Sotomayor, wawili kati ya majaji watatu wa kiliberali wa mahakama hiyo, walipinga.

    Utawala wa Trump ulikuwa umewasilisha rufaa ya dharura kwa Mahakama ya Juu baada ya jaji wa shirikisho huko Massachusetts kuzuia utawala kusitisha mpango huo, unaojulikana pia kama msamaha wa kibinadamu wa CHNV.

    Ikulu ya White House "ilisherehekea" fursa ya kuwafukuza "wavamizi" 500,000, Naibu Mkuu wa Wafanyakazi wa Ikulu ya White House Stephen Miller aliambia CNN. "Mahakama ya Juu iliingia kwa haki".

    Soma hapa zaidi:

  8. Wagonjwa waondoka katika Hospitali ya mwisho katika jimbo la Gaza Kaskazini baada ya agizo la Israel

    g

    Chanzo cha picha, al-Awda staff

    Maelezo ya picha, Picha ya skrini kutoka kwenye video iliyotolewa na wafanyakazi wa hospitali, inaonyesha watu, wengine wamevaa fulana zenye jina la hospitali mgongoni, wakibeba mabegi kwenye gari la wagonjwa.

    Hospitali ya mwisho inayotoa huduma za afya katika eneo la Gaza Kaskazini haifanyi kazi baada ya jeshi la Israel kuamuru kuhamishwa mara moja kwa wagonjwa nashughuli zake, mkurugenzi wa hospitali hiyo amesema.

    Dkt Mohammed Salha aliiambia BBC wagonjwa walihamishwa kutoka hospitali ya al-Awda huko Jabalia Alhamisi jioni baada ya "wiki mbili za kuzingirwa", na sasa "hakuna kituo cha afya kinachofanya kazi kaskazini".

    Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) bado halijajibu lolote kuhusiana na hatua hiyo.

    Hii inakuja huku juhudi zikiendelea kufikia usitishaji mapigano. Hamas inasema "inapitia kwa kina" mpango wa Marekani, ambao Ikulu ya Marekani imesema "umetiwa saini" na Israel.

    Rais wa Marekani Donald Trump alisema siku ya Ijumaa anaamini makubaliano yalikuwa "karibu sana". Lakini Hamas imesema mpango huo haukidhi matakwa yake ya msingi ikiwa ni pamoja na kujitolea kwa Israel kumaliza vita.

    Makubaliano hayo yanaripotiwa kuhusisha kusitisha mapigano kwa siku 60, huku Hamas ikiwaachilia mateka 28 - wakiwa hai na wamekufa - katika wiki ya kwanza, na mateka 30 waliosalia wakiachiliwa mara tu usitishaji wa kudumu wa mapigano utapoanza.

    Kufuatian makubaliano hayo zaidi ya wafungwa 1,000 wa Kipalestina wataachiliwa, na misaada ya kibinadamu ikitumwa Gaza kupitia Umoja wa Mataifa na mashirika mengine kutolewa .

    Israel imeendeleza operesheni yake ya kijeshi katika eneo hilo na takriban watu 72 waliuawa katika mashambulizi katika muda wa saa 24 zilizopita, wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas ilisema Ijumaa.

    Unaweza pia kusoma:

  9. Hujambo na karibu kwa matangazo haya ya mubashara Jumamosi hii ya tarehe 31.05.2025, tukikuletea habari za kikanda na kimataifa.