Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Madrid, Liverpool zapigana vikumbo kwa Wirtz

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid wanaharakisha kumsajili winga wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz, sasa ambapo kocha wake wa zamani Xabi Alonso ametangazwa kuwa kocha mpya wa Los Blancos, licha ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 22 kuhusishwa zaidi na Liverpool. (AS)
Newcastle wako tayari kutoa ofa za kwasajili beki wa Crystal Palace na England, Marc Guehi, 24, na mshambuliaji wa Cameroon mwenye umri wa miaka 25 wa Brentford, Bryan Mbeumo katika majira ya joto. (Telegraph)
Brentford wameifuata Liverpool kuhusu kumsajili kipa wao Caoimhin Kelleher, 26, ambaye anathamani ya pauni milioni 20. (Liverpool Echo)
Hatua ya kumsajili Kelleher inakuja wakati Brentford wanajiandaa kumruhusu kipa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 31, Mark Flekken, kujiunga na Bayer Leverkusen. (Independent)

Chanzo cha picha, Getty Images
Bayern Munich wanavutiwa na mshambuliaji wa Liverpool, Cody Gakpo, 26, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikiwa moja ya timu tatu ambazo mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi ananaweza kukubali kujiunga na moja wapo (Florian Plettenberg)
Beki wa pembeni wa Bournemouth, Milos Kerkez, tayari amekubali kujiunga na Liverpool na hakuna wasiwasi kuhusu masharti binafsi kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Hungary mwenye umri wa miaka 21. (Fabrizio Romano)
Wakala wa mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford, alikutana na mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Deco, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 27 akitamani sana kujiunga na mabingwa hao wa La Liga. (Sport)
Arsenal wamelenga kumsajili winga wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 29, Leroy Sane, ambaye mkataba wake unamalizika Bayern Munich msimu huu wa joto. (Times)

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle ni moja ya vilabu vinavyofanyia kazi dili la kumsajili mshambuliaji wa Ipswich Town, Liam Delap, 22, ambaye pia ana ofa kutoka Chelsea, Manchester United na Everton. (ipaper)
Arsenal wameambiwa na RB Leipzig wanapaswa kulipa pauni milioni 92.5 ili kumsajili mshambuliaji wa Slovenia mwenye umri wa miaka 21, Benjamin Sesko, ambaye pia anasakwa na Manchester United.
Kiungo wa England, Jordan Henderson, 34, anaweza kuondoka klabu ya Uholanzi Ajax na kurudi kwa kushangaza kwenye klabu yake ya nyumbani Sunderland msimu huu wa joto. (Mirror)
Mabingwa wa Italia, Napoli, wako tayari kukamilisha usajili wa bure wa Kevin de Bruyne, 33, na mshambuliaji wa Canada mwenye umri wa miaka 25, Jonathan David, kujiunga na klabu hiyo ya Serie A mikataba yao itakapomalizika kwenye vilabu vyao vya Manchester City na Lille mwezi ujao. (Corriere dello Sport)
Roma wako karibu kumteua Gian Piero Gasperini kuwa kocha wao mpya baada ya Muitaliano huyo kuondoka Atalanta baada ya miaka tisa ya kukinoa kikosi hicho (Gazzetta dello Sport)